Wednesday, 1 October 2014


Kila mwaka kuanzia tarehe 1 ya mwezi Oktoba hadi tarehe 5 dunia huwa inaazimisha siku ya walimu duniani. Iringa nayo haikuwa nyuma kwani leo tarehe 01/10/2014 iliadhimisha sherehe hiyo ambayo ilianza kwa maandamano yaliyoanza ofisi za Manispaa Iringa na kuishia katika uwanja wa Samora ulioko katika Manispaa ya Iringa.

Sherehe hizo ambazo zilipambwa na shamrashamra mbalimbali zikiwemo ngoma, nyimbo, mashairi na maigizo ambayo yalifanywa na walimu wenyewe ilikuwa ni ya kupendeza sana. Katika sherehe hiyo ambyo naibu waziri wa elimu alitakiwa kufika na kuwa mgeni rasmi hakuweza kufika na matokeo yake aliweza kuwakilishwa kwani wakuu wa idara karibu wote Tanzania wapo Dodoma kwa kazi maalumu. Zifuatazo ni picha za shamrashamra hizo kama zilivyopigwa na mwakilishi wa Fema kutoka Iringa Zoo

No comments:

Post a Comment