Wednesday, 1 October 2014

Hawa ni viongozi wa PSA yaani Umoja wa Wanafunzi wa Kipentekoste ambao walichaguliwa Jumapili ya tarehe 28/09/2014 kuongoza tawi la Iringa Girls baada ya uongozi ambao ulikuwa ukiongozwa na mwenyekiti Anna Kaguo kustaafu baada ya kutumika kwa muda wa mwaka mmoja. Tunawatakia uongozi mwema na Mungu awabariki katika kuchaguliwa kwenu na muifanye kazi ya Mungu ipasavyo hapa shuleni Iringa Zoooooooooooo



Kila mwaka kuanzia tarehe 1 ya mwezi Oktoba hadi tarehe 5 dunia huwa inaazimisha siku ya walimu duniani. Iringa nayo haikuwa nyuma kwani leo tarehe 01/10/2014 iliadhimisha sherehe hiyo ambayo ilianza kwa maandamano yaliyoanza ofisi za Manispaa Iringa na kuishia katika uwanja wa Samora ulioko katika Manispaa ya Iringa.

Sherehe hizo ambazo zilipambwa na shamrashamra mbalimbali zikiwemo ngoma, nyimbo, mashairi na maigizo ambayo yalifanywa na walimu wenyewe ilikuwa ni ya kupendeza sana. Katika sherehe hiyo ambyo naibu waziri wa elimu alitakiwa kufika na kuwa mgeni rasmi hakuweza kufika na matokeo yake aliweza kuwakilishwa kwani wakuu wa idara karibu wote Tanzania wapo Dodoma kwa kazi maalumu. Zifuatazo ni picha za shamrashamra hizo kama zilivyopigwa na mwakilishi wa Fema kutoka Iringa Zoo

Tuesday, 30 September 2014


Tutawakumbuka viongozi wetu wastaafu wa FEMA hapa Iringa Zoo. Poa mkajitolee huko uraiani na mtukumbuke


Mwalimu mlezi wa Iringa Zoo Fema Club Mwl.Gaudence John Mhando


Wa kwanza kutoka kushoto ni makamu mkuu wa shule Mwl.Kabula, katikati ni mgeni rasmi ni lecturer kutoka Iringa University na wa mwisho ni mkuu wa shule Iringa Girls Mwl.Msigwa wakumsikiliza kwa makini mwenyekiti wa Iringa zoo Fema Club Haika (Hayupo pichani) akieleza mikakati ya club ya Fema hapa Iringa Girls

Miongoni mwa mabango ambayo yalionekana kwenye chumba cha maonyesho cha Fema siku ya Academic and Carrier Day. Mchoro ambao wameutoa kwenye jarida la July-September 2014 uk.57 na mchoraji akiwa ni katibu wa Iringa Zoo Fema club Honoratha Gutram